Merkel asema vikwazo vya COVID-19 vitaendelea hadi Januari 2021




Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema nchi hiyo italazimika kuendelea na hatua walizoweka kukabiliana na kusambaa kwa virusi vya corona hadi mwezi Januari
Merkel ameliambia leo bunge la Ujerumani kuwa, kutokana na idadi kubwa ya maambukizo ya ugonjwa wa COVID-19, vikwazo ambavyo vilikuwa vimewekwa awali vitaendelea kuwepo hadi mwanzoni mwa mwezi Januari.

Kauli yake inaonekana kuungwa mkono na mkuu wa utumishi katika ofisi yake aliyependekeza kuwa vikwazo hivyo viendelee kuwepo hadi mwezi Machi.

Hapo jana, Merkel alikubaliana na wakuu wa majimbo 16 ya Ujerumani kuendelea kuweka vikwazo hadi Desemba 20, na kulegeza vikwazo hivyo baada ya hapo ili kuruhusu watu kusheherekea likizo zao wakati wa sikukuu ya Krismasi


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad