Kwa miaka mingi, Shiva amekuwa akisadia polisi kupata miili ya watu katika ziwa Hussain Sagar kusini mwa India mji wa Hyderabad.
Siku moja alimuokoa mtu kabla ya kuruka majini na kunusuru maisha ya mtu kwa mara ya kwanza. Mwanahabari wa BBC wa Telugu Balla Satish amesema.
Shiva, ambaye anatumia jina moja anasema alikuwa na umri wa miaka 10 alipokutana na kundi la polisi ambao walijitolea kumlipa mtu yeyote ambaye angeweza kuopoa mwili karibu na kidimbwi.
Polisi nchini India wanalipwa pesa kidogo na mafunzo wanayopewa pia ni duni.
Wengi wao hawajui namna ya kuogelea na pia hawapewi pesa ya kutafuta wapiga mbizi wenye utaalamu.
Kwahiyo imekuwa kawaida wao kutegemea waogeleaji wasio na utaalamu.
Lakini Shiva alipojitolea, anasema, walishtuka. “Mwanzo, walikataa wakisema kwamba umri wangu ni mdogo sana. Lakini nikawashawishi hadi wakakubali,” anakumbuka.
Alifanya kazi hiyo na kulipwa rupee 40, ambazo kwa sasa ni sawa na karibu dola 0.54 lakini wakati huo haikuwa pesa kidogo hivyo kwake.
Hiyo ilikuwa ni miaka 20 iliyopita. Sasa hivi ana umri wa miaka 30 na bado anasaidia polisi wa eneo.
Shiva anaishi karibu sana na mto mkubwa unaofahamika kama Hussain Sugar.
Eneo hilo ni kivutio cha utalii na ziwa hilo pia linatumika wakati wa tamasha la Ganesha la kuzamisha masanamu majini ambayo Wahindi wanayachukulia kama miungu wao.
Lakini pia eneo hilohilo ni sehemu ambayo wengi hupoteza maisha yao na mara nyingi Shiva anasaidia polisi kuopoa miili ndani ya maji.
Wakati mwingine, pia huwasaidia kupata miili kutoka kwa mito na maziwa mingine katika mji.A 18-meter high Buddha statue stands in the middle of Hyderabad's Hussain Sagar lake.
Shiva anafanya mengi zaidi ya kuopoa miili kutoka kwenye ziwa – mara nyingi huokoa watu kabla hawajajirusha majini, na wakati mwingine hata baada ya kujirusha.
“Siwezi kuhesabu ni miili mingapi nimeiopoa. Lakini hadi kufia sasa nimenusuru maisha ya watu 114,” ameiambia BBC.
Sasa hivi anamfundisha mke wake kuogelea ili naye aweze kusaidia kuopoa miili ndani ya maji.
Inspekta B Dhanalakshmi, ambaye anafanyakazi katika kituo cha polisi karibu na ziwa Hussain Sagar, anatambua kuwa Shiva amekuwa wa “msaada mkubwa” kwao.
“Siwezi kuthibitisha ni watu wangapi amechangia kunusurika kwao lakini naamini ni zaidi ya watu 100,” ameiambia BBC.
Kujitoa uhai bado ni uhalifu nchini India na wengi ambao Shiva hunusuru maisha yao, hukimbia hata kabla hajapiga simu kuita polisi.
Shiva anasema hajui wazazi wake na muda mwingi maishani mwake akiwa mtoto alikuwa akiishi mitaani, huku akisikia kuwa yeye ni mtoto yatima.
Ilifika wakati – hakuwa na uhakika ana umri wa miaka mingapi – alianza kuishi na mama mmoja mwenye watoto wake ambaye pia naye alikuwa hana makazi. Alikuwa karibu sana nao na mmoja wa vijana wake ndio walimfundisha kuogelea, ujuzi uliobadilisha kabisa mkondo wa maisha.
“Nimepoteza rafiki wengi kwa miaka kadhaa – kwasababu ya uraibu, baa la njaa na hata ajali,” anasema. Mvulana aliyemfunza kuogelea – “kaka yangu Lakshman,” anavyomuita – kwa bahati mbaya alizama majini na rafiki yangu mwingine wa karibu wakijaribu kumnusuru mtu.
Anasema kwasababu hakuweza kuwaokoa, anajitahidi kulifidia hilo kwa kunusuru wengine.
Kunusuru maisha kunamfanya kupata pesa za ziada – wakati mwingine wale anaowaokoa humpa kiinua mgongo kama shukrani.
Na pia kuangaziwa na vyombo vya habari kumemfanya kuwa mashuhuri na kuchangia kupata fursa ndogo ndogo za uingizaji filamu Telugu.
Lakini Shiva anasema hachukulii kunusuru watu kama kazi.Indian devotees watch as crane workers immerse an idol of Hindu deity Ganesh in the Hussain Sagar Lake on the eleventh day of the Ganesh Chaturthi festival in Hyderabad on September 23, 2018.
Sababu za watu kutaka kujiua, anasema, zinatofautiana kuanzia shinikizo la mtihani ya maisha, suala la mapenzi kwenda mrama hadi masuala ya kifamilia na matatizo ya kifedha.
Anasema mara nyingine watu wazima hujaribu kujiua wanapotelekezwa na wazazi wao.
Anasema, hivi karibuni aliona mwanaume akijirusha kwenye ziwa kwa kuhofia kuwa huenda akawa amepata maambukizi ya virusi vya corona.
Rafiki ya mtu huyo aliruka majini akijaribu kumnurusu kabla ya Shiva pia naye kuwafuata kwa kuruka majini ingawa alifanikiwa kumnusuru rafiki yake pekee.
Anasema familia ya mwanaume huyo aliyefariki dunia, hata haikuwahi kuuchukua mwili wake ikihofia kuwa huenda pia nao wakapata maambukizi ya virusi vya corona.
“Kwa hiyo nikaamua kumchoma moto,” anasema.
“Nilimuokoa mwanaume mwingine ambaye alisema familia yake imeanza kumnyanyapaa kwasababu inafikiria kuwa amepata maambukizi ya virusi vya corona.”Shiva jumping into the lake
“Hakuna muda wa kuvaa vifaa vingine vya kujikinga. Unahitajika kuchukua hatua ya haraka. Unapomuona mwingine anajirusha majini, kinachohitajika kufanyika ni pia nawe uruke wakati huohuo.”
“Nataka kuishi hapa,” anasema. “Kuishi kwangu hapa tu ndio kunaweza kunifanya kunusuru maisha. Unachohisi wakati umeokoa maisha ya mtu, kunatosheleza.”
Hata hivyo kazi ya Shiva, inakuja na gharama zake.
Ziwa Hussain Sagar umechafuliwa vibaya na Shiva ambaye mara kwa mara huingia kwenye ziwa hilo bila kuvaa vifaa stahiki anasema ameanza kuwa na harara pamoja na magonjwa mingine ya ngozi.