England inapaswa kumuachisha kazi, Gareth Southgate na nafasi yake kuchukuliwa na kocha sahihi kama Jose Mourinho, amesema Ahmed Hossam Hussein maarufu kama Mido huku akimpendekeza Mreno huyo kuchukua kibarua cha Southgate.
Gareth Southgate is not the man to lead England forward as manager, according to Mido
Mmisiri huyo ambaye amewahi kucheza chini ya Southgate ndani ya klabu ya Middlesbrough amemuwasha kocha huyo wa Three Lions baada ya timu yake ya England kupokea kichapo cha jumla ya goli 2 – 0 dhidi ya Ubelgiji kwenye michuano ya Nations League hapo jana siku ya Jumapili.
Southgate managed Mido at Middlesbrough but the former striker evidently does not rate him
Mido ameandika kuwa England inahitaji kocha sahihi ”England inahitaji kocha sahihi, wanapoteza muda wao kuendelea kuwa na Southgate.”
”Ni kweli kuwa siku zote anazungumza ukweli mbele ya vyombo vya habari na pengine ndiyo sababu ya anafanikiwa kuilinda kazi yake kwa muda mrefu sasa lakini niamini amekuwa mwenye kigugumizi kila pale mambo yanapokwenda hovyo, na wachezaji wamekuwa wenye hofu.” amesema Mido.
Mchezaji huyo aliyekuwa akicheza safu ya ushambuliaji katika klabu alizowahi kupitia ameongeza ”Namkumbuka sana nilivyokuwa naye Middlesbrough, alikuwa mwenye hofu kufa wakati tulipokuwa tukipambana tusishuke daraja. Ukweli ilikuwa kazi yake ya kwanza lakini hivi vitu havibadiliki. Kama utakuwa mwenye hofu ya kupoteza katika mechi hata wachezaji wako watakuwa na hisia hizo.
”England imebarikiwa kuwa na vijana wenye vipaji lakini inahitaji kocha mwenye imara mtu ambaye atawafanya wafurahie na watakaocheza bila hofu.