Miili ya watu 103 yagundulika kwenye kaburi la halaiki lililofukuliwa Mexico

 


Kulingana na taarifa iliyochapishwa na vyombo vya habari vya nchi, Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali ilisema kwamba miili 103 iligunduliwa kwenye kaburi la halaiki wakati wa shughuli ya utafutaji iliyofanyika katika uwanja wa  El Salto ulioko Jalisco.

Katika ukaguzi wa kwanza uliofanyika juu ya miili hiyo, watu 30 wakiwemo wanawake wawili miongoni mwao waliweza kutambuliwa na familia zao.


Shughuli ya ukaguzi ili kuitambuliwa miili mingine pia inaendelea.


Kwa mujibu wa ripoti iliyochapishwa mwezi Oktoba na Tume ya Kitaifa ya Utafutaji ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Mexico, miili 897 ilipatikana katika makaburi ya siri yaliyogundulika wakati wa ukaguzi huko Jalisco kati ya mwaka 2006-2020.


Kwa upande mwingine, katika ukaguzi uliofanywa tangu 2006 nchin humo, jumla ya miili ya watu 6,900 ilipatikana kwenye makaburi 4,092 ya siri yaliyofukuliwa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad