Mke wa Donald Trump, Melania Trump amejiunga na kikosi cha ushauri cha rais huyo kumshawishi kukubali ushindi wa Biden na pia kukubali kushindwa.
Vyanzo vya karibu na Mwanamama huyo vimeiambia CNN kuwa, Mama wa taifa ambaye bado hajatoa maoni yake kuhusu matokeo ya uchaguzi hadharani amesema wakati umefika kwa mume wake kukubali kushindwa.
Mbali na Melania, mkaza mwana wa Trump na mshauri wake mkuu Jared Kushner pia Wamemhimiza akubali matokeo.
Aidha, Donald Trump Junior na Eric Trump kwa upande wao wanamshauri baba yao kupinga matokeo na kutaka chama cha Republican kujitokeza hadharani kukataa matokeo hayo.
Kiongozi huyo wa chama cha Republican ambaye anapania kuchaguliwa kwa muhula wa pili alisema atakosoa matokeo hayo kwenye Mahama Kuu. Akizungumza siku ya Jumatano, Novemba 4, kutoka Ikulu ya White House, Trump aliwataka wafuasi wake kujiandaa kusherehekea ushindi wake.
“Kuna udanganyifu, hii ni aibu kwa Marekani, naenda Mahakamani ili mchakato wa upigaji kura usimame hatutaki zikutwe kura asubuhi na kura zinaongezwa kwenye orodha” alisema Trump.