Mo Dewji Amaliza Utata Chama na Mukoko



Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya klabu ya Simba Mohammed Dewji, amethibitisha kuwa mchezaji Clatous Chama, amesaini mkataba wa miaka miwili zaidi na klabu hiyo, awali kulikuwa na tetesi kuwa huenda angesajiliwa na watani zao Yanga.


Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es salaam, leo Novemba 15, 2020 Mo Dewji amesema Chama hataenda kokote kwa misimu miwili na nusu ijayo.


“Sisi Simba tumejipanga. Chama hajaenda popote, tumeshasaini naye mkataba na atabaki na Simba. Tumemalizana na Chama na ni mchezaji wa Simba kwa miaka miwili na nusu ijayo.” amesema.


 


Aidha Mo Dewji amekanusha tetesi za kutaka kumsajili kiungo wa klabu ya Yanga SC, Tonombe Mukoko ambapo amesema hawajawahi kujadili suala hilo.


 


”Kuhusu suala la Simba kumsajili Tonombe Mukoko, kusema ukweli hata kwenye bodi hatujaliongelea, ni propaganda tu watu wameanzisha na hakuna taarifa rasmi ya Simba kama huyo mchezaji tunamtaka, tunachofanya ni kusikiliza kocha anasema wapi kuna mapungufu na tunayafanyia kazi”.


 


Na kuhusu  kiungo wa Kibrazili Gerson  Fraga, Mo Dewji amesema, ”Mchezaji wetu Mbrazil  amepata majeruhi yatakayomuweka nje muda mrefu, hivyo kwenye dirisha dogo hili kwa mapendekezo ya mwalimu tutamtafuta mchezaji atakaye ziba pengo hili’.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad