HitMaker wa nyimbo za basi nenda na nitazoea Mo Music amefunguka kuwa asilimia 90 ya wasanii wa hapa Bongo wanawajua waganga na hata yeye aliwahi kwenda kwa ajili ya kutibiwa mguu pia anaamini kwenye u-Afirca zaidi.
Mo Music amesema alienda kwa mganga kwa sababu aling'atwa na nyoka mguuni hivyo akaenda kupatiwa tiba pia alishawahi kumpeleka mtu mwingine ambaye alikuwa na matatizo ya akili.
"Nimewahi kwenda kwa mganga ila nilikuwa naumwa mguu na niling'atwa na nyoka, karibia asilimia 90 ya wasanii wote wanamjua mganga lakini kikubwa ni kuangalia juhudi zako, pia niliwahi kwenda kwa ajili ya kumpeleka mtu ambaye alikuwa ana matatizo ya akili, sisi tunaamini kwenye u-Afrika bana" amesema Mo Music