Kijana mwenye ulemavu wa miguu, Melchedek Lyimo (28), amefariki dunia baada ya nyumba aliyokuwa akiishi na mama yake mzazi kuteketea kwa moto uliowashwa na mama yake ili kuua siafu.
Tukio hilo ambalo limeacha simanzi na majonzi makubwa katika Kijiji cha Kyou wilayani hapa Mkoa wa Kilimanjaro, lilitokea saa 7 usiku wa kuamkia jana.
Mama mzazi wa kijana huyo, Anna Didas (68), alijeruhiwa na moto huo, wakati akijaribu kumuokoa mtoto wake ambaye alikuwa hawezi kutembea kutokana na ulemavu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Emmanuel Lukula, alipoulizwa na gazeti hili jana kuhusiana na tukio hilo, alisema hajapata taarifa hizo lakini diwani wa Kata ya Kilema Kaskazini, Anna Lyimo alithibitisha.
Alisema alipigiwa simu na mwenyekiti wa kitongoji na alipofika alikuta tayari mama wa marehemu ameshakimbizwa hospitali na wao kubaki kufanya taratibu za kukusanya mabaki ya marehemu.
Frank Raphael ambaye ni jirani wa familia hiyo, alisema baada ya kuona moto huo, alitoka kwenda kutoa msaada na alipofika alimkuta mama huyo akikazana kumvuta mwanae aliyekuwa akiungua