Staa wa muziki kutoka nchini Zimbabwe, Ngonidzashe Dondo maarufu kama @king98official amefunguka ni namna gani ameweza kukutana na msanii wa muziki Diamond na kufanya kolabo iitwayo ‘KACHIRI’
Kupitia mahojiano aliyofanya hivi karibuni King98, ameleza kuwa tayari ameshafanya kazi na wasanii kutoka Ukanda wa Afrka Magharibi kama vile @davido na mastaa wengine hivyo, CEO wa DMW akamshauri sasa afanye na staa kutoka Afrika Mashariki ambaye ni @diamondplatnumz Baada ya ushauri huo ndipo Davido na team wakamtafuta Diamond Platnumz kwa ajili ya kolabo.
“Nilikutana na Diamond kupitia Davido, nilikuwa na nyimbo na wasanii kutoka Kusini, Katikati na Magharibi mwa Afrika kasoro Afrika Mashariki, Nilimtafuta Diamond na akapenda wimbo wangu na tukakutana tukafanya kazi. Nilijua ni mtu wa majivuno ila nilipokutana naye ni mtu mkarimu, mpole na mwenye upendo wa hali ya juu” ameeleza King98
Pia msanii huyo ameeleza kuwa mpaka sasa ameshafanya kolabo na wasanii kama Rayvanny, Zuchu na Jux ambao watasikika kwenye album yake ijayo inayotarishwa pia na producer S2kizzy.