Mbuzi maarufu wa Msumbiji amepewa cheti maalumu kama sehemu ya mipango ya kuulinda utambulisho wake atakaposafirishwa nje ya nchi kuuzwa kwenye soko la dunia.
Waziri wa viwanda na biashara nchini humo, Carlos Mesquita, ameyasema hayo akiongeza kuwa, ishara ya utambulisho wa kijiografia katika nyama ya mbuzi utahakikisha sifa ya ubora wake inalindwa.
Mbuzi huyo aina ya Tete yana umuhimu wa kipekee katika Msumbiji, kwasababu ya nyama yenye utamu wa kipekee.
Nyama ya mbuzi inaweza kuliwa wakati wote nchini Msumbiji, lakini mara kwa mara huliwa katika sherehe za kitamaduni na kijamii, mkiwemo harusi na katika sherehe za mahafari.
GI ni cheti kinachothibitisha kwamba bidhaa fulani inatoka katika eneo fulani linalofahamika kwa ubora wake, ikimaanisha kuwa bidhaa kutoka maeneo mengine hayawezi kutumia jina sawa na hilo – sawa na inavyofanyika katika pombe aina ya Champagne.