Mtandao wa wezi wa watoto Kenya wakamatwa



Polisi nchini Kenya imesema kuwa imebaini mtandao unaohusika na wizi wa watoto katika jiji la Nairobi.

Sakata hii imebainika baada ya kipindi cha uchunguzi cha BBC Africa Eye kupeperushwa hewani ambacho kilionesha uhalifu unaotendeka katika maeneo mbalimbali na hospitali za umma.


Maafisa watatu wa matibabu wa hospitali za umma wamekamatwa na polisi na imedokeza kuwa bado kuna wengi ambao wanatafutwa.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Inspekta Generali wa polisi Hillary Mutyambai, ilisema uchunguzi na taarifa kutoka kwa washirika umeonesha maafisa waandamizi wa matibabu wanahusika kwa kiasi kikubwa na wizi wa watoto.


Taarifa hiyo ilisema hospitali za umma na makao ya watoto ndani ya jiji la Nairobi pia vinahusika katika sakata hiyo.


Inspekta Mutyambai ameagiza makamanda wa polisi mjini Nairobi kufanya uchunguzi mara moja katika hospitali za umma na za kibinafsi pamoja makazi ya watoto.


Agizo hilo linakuja siku mbili tu baada ya kipindi cha BBC Afrika Eye kupeperusha makala iliyoweka wazi jinsi mitandao haramu inavyofaidika na wizi wa watoto ambao huuzwa hata kwa pesa kidogo tu ya dola 450 za Marekani.








OPEN IN BROWSER

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad