Mwanamke anayeitwa Gladys anapata matibabu katika hospitali ya Orerokpe iliyopo katika jimbo la Delta , kusini mwa Nigeria, baada ya mume wake kumfungia ndani ya seng’enge kwenye chumba chake kwa muda wa miaka minne.
Harrison Governor, ambaye alikuwa mmoja wa watu waliofichua tukio hili aliiambia BBC jinsi mume wake Gladys alivyomfungia kwenye kichumba kidogo kilichopo katika eneo la nyumba yao kwasababu alimtuhumu kuwa mchawi.
Gladys aliokolewa kutoka kwenye eneo hilo hilo lililofungwa Jumatano, na ilifichuliwa kuwa alikuwa akijisaidia mahali hapo haja ndogo na kubwa na kupewa kipande kimoja cha mkate pekee kama chakula cha siku nzima.
Gladys kwa sasa yuko katika hospitali ya Orerokpe Hospital ambako anapokea matibabu.
Kufungiwa ndani ya pango kwa Gladys
Harrison anasema Gladys alikuwa na watoto wanane, na watatu walifungwa pamoja naye katika chumba hicho.
“Jina lake ni Gladys, na anatoka katika kabila la Ozoro kutoka jimbo la Delta , na anaonekana kuwa na umri wa miaka 40 na zaidi…hayuko katika hali nzuri kwasababu tangu jana hajaweza kuzungumza lolote .
“Lakini tunataka kumpeleka hospitalini ili afanyiwe vipimo. Mume wake kwa sasa yuko katika kituo cha polisi .”
Harrison aliongeza kuwa kwa sasa, Waziri wa masuala ya wanawake katika jimbo la anawatunza watoto wake wa kike kwasababu bado ni wadogo sana.
Aliongeza kuwa wakati mama yao akihudumiwa kabla hajapona, wataangalia jinsi ya kupeleka kesi kwa idara ya upelelezi wa makosa ya jinai ya jimbo.
Gladys for hospital
Mume wake Gladys alikamatwa
Msemaji wa polisi katika jimbo la Delta Onome Umukoro aliithibitishia BBC tukio hilo, akisema kuwa mume wake Gladys tayari yuko mikononi mwa polisi na anaendelea kufanyiwa uchunguzi.
Umukoro alieleza kuwa mume wa Gladys alikuwa amewaambia kuwa Gladys ana matatizo ya kiakili na kwamba anashutumiwa kuwa mchawi, ndio maana bado alikuwa anaishi nae.
Amesema alijaribu kuwatembelea waganga mbalimbali wa kienyeji ili wamtibu lakini ilishindikana.
Pia alisema kuwa alimrudisha katika familia yake lakini walimkataa na wakakataa kumkubali kwahiyo alilazimika kumrudisha nyumbani na kuendelea kuvumilia kuishi nae.