Daktari bingwa wa afya ya akili na uraibu wa dawa za kulevya wa Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala, Dk. Sostesjofu Mongu ameeleza unywaji wa pombe unaofaa kiafya ili kuepukana kuwa tegemezi na magonjwa yasiyoambukiza.
Kwa mujibu daktari huyo kiafya mwanamke anashauriwa kunywa chupa saba za bia kwa wiki moja huku mwanaume akishauriwa kunywa chupa 14 za bia kwa wiki moja.
Dk. Mongu amesema pombe ni kilevi chochote ambacho mtu akinywa kinabadilisha mtazamo, hisia na mawazo ya mnywaji.
“Kiwango cha ulevi wa pombe inategemea na ujazo wa pombe kuna za mill 100, zingine 250 hadi 500 kwahiyo kila pombe ina ujazo wake na kiwango cha ‘alcohol’ inategemea na aina ya pombe” Dk. Mongu
“Tunasema kuna aina ya unywaji ambao unaboresha afya huu ni unywaji usiokuwa na madhara kwa lugha nyepesi tunaita unywaji wenye afya ambao unaboresha mzunguko wa damu” Dk. Mongu
“Kwa mwanamke kwa wiki moja anatakiwa asinywe zaidi ya chupa saba za bia na kwa mtoko mmoja anatakiwa kunywa chupa moja hadi tatu tu na kwa mwanaume kwa wiki asizidi chupa 14 na kwa mtoko mmoja anatakiwa kunywa chupa mmoja mpaka nne huo ndio unywaji salama kwa afya” Dk. Mongu