Mwaume mmoja kutoka Kaunti ya Kericho nchini Kenya amewashangaza wengi na kuibua gumzo mitandaoni baada ya kudaiwa kufufuka akiwa katika chumba cha maiti saa chache baada ya kupelekwa kwenye chumba hicho.
Kulingana na mjomba wake Denis Langat, mwanaume huyo ambaye anajulikana kama Peter Kiplangat alipelekwa hospitalini Jumanne asubuhi baada ya kupoteza fahamu akiwa nyumbani lakini akathibitishwa kufa alipofikishwa hospitalini.
Kulingana na mjomba wake, Peter alishituka na kupiga mayowe baada ya muhudumu wa chumba cha kuhifadhia maiti kupasua sehemu ya paja, mojawapo ya mchakato ambao hufanywa kama njia moja ya kuuhifadhi mwili unapowekwa kwenye chumba cha maiti.
Hapo ndipo mhudumu huyo alipokimbia na kumuita daktari.
Akizungumza na waandishi wa habari katika kaunti ya Kericho, daktari mkuu wa Kapkat, Gilbert cheruiyot, amesema kuwa Denis Langat alifikishwa hospitalini akiwa amepoteza ufahamu, Lakini jamaa zake walipoona kuwa wauguzi wanachukua muda kuwashughulikia, wakampeleka katika chumba cha mauti.
“Wakati mhudumu wa chumba cha kuhifadhia waliona kwamba bado mgonjwa yuko hai, waliwaita wahudumu wengine waje wamzindue.
Kwa sasa ndugu wa Denis Langat wanadai haki Kwa kuishutumu hospitali kutowajibika.