No title



Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba, Mohammed Dewji amemalizana na mwanachama wa Simba, Hamisi Kigwangalla baada ya wawili hao kutupiana maneno ya hapa na pale kwenye mitandao ya kijamii yaliyokuwa yakihusisha uwekezaji wake kuelekea mfumo wa mabadiliko ndani ya klabu hiyo.

KIGWANGALLA AOMBA YAISHE KWA MO ~ Bin RUWEHY

Mo Dewji kupitia mitandao yake ya kijamii amesema kuwa wote wana mapenzi ya dhati na Simba, na kutumia nafasi hiyo kuomba radhi pale alipokosea na yeye kwa upande wake alipokosewa na Kigwangalla amesamehe.

”Nia njema ni tabibu, nia njema ni ibada. Sote tuna mapenzi ya dhati na Simba, hata tulipokwazana ilikua katika nia njema kwenye maendeleo ya timu yetu. Naomba radhi nilipokosea na mimi uliponikosea nishasamehe. Tuijenge Simba pamoja sasa.” ameandika Mo Dewji

Juma lililopita kwa upande wake Dkt. Hamisi Kigwangalla alitumia mtandao wake wa kijamii kuomba radhi kwa yaliyotokea kama hivi leo Dewji anavyofanya.

”Wanasimba tunataka ushindi dakika 90 uwanjani na mchango wa Mohammed siyo wa kudharau kwenye hili, lakini hata yeye na biashara zake wanafaidika na Simba as a brand, siyo bure tu. Thamani ya Simba siyo majengo, ni brand yenye umri wa zaidi ya miaka 80. Tanzania ni lazima uwe Simba ama wale wengine…hata kama unamiliki timu yako. Siyo kitu kidogo. Simba ina maslahi ya umma. Ninaweza kusema mengi lakini siyo lengo langu. Nimekuwa nikiwaza juu ya kusameheana. Yaishe. Tusonge mbele. Naomba radhi kwake na kwa washabiki wote wa Simba niliowakwaza. Mimi nimesamehe. Maisha,” sehemu ya maandishi ya Dkt. Hamisi Kigwangalla akiomba radhi.

Wawili hao ambao wote ni wanachama wa miamba ya soka Afrika Mashariki Simba SC walizua gumzo mitandaoni baada ya kujibizana kuhusiana na uwekezaji ndani ya timu hiyo.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad