Beki wa kushoto wa zamani wa Yanga, Haji Mwinyi Mngwali amesema kikosi cha timu yake ya zamani kipo vizuri kwa sasa, hivyo wakipambana zaidi wanaweza kutwaa ubingwa.
Mwinyi aliyasema hayo alivyohojiwa leo tarehe 16/11/2020 na Zainabu Rajabu Kipenga ya East Africa Radio
''Nimekuwa Yanga kwa muda mrefu,nimefanikiwa kutwaa ubingwa, mara tatu tulikuwa na kikosi bora sana, miaka miwili iliyopita timu hii haikuwa na kikosi bora, ukilinganisha na kikosi hichi cha sasa hivyo wakikaza tu, ubingwa wao''alisema Mwinyi
Mwinyi alisajiliwa na Yanga mwaka 2015 akitokea KMKM ya Zanzibar, na kudumu hadi 2018 akiwa mchezaji wa kutumainiwa katika safu ya ulinzi, mpaka alipowasili kocha Mwinyi Zahera ambapo hakuingia katika filosofi yake ya mchezo na hatimaye kuachwa katika usajili,
Baadaye akalazimika kutimukia Singida Utd, hata hivyo timu hiyo baadaye ilishuka daraja na kwa sasa anacheza timu yake ya zamani ya KMKM ambayo ipo hapa Dar-es-salaam kwa ziara ya michezo kadhaa wa kirafiki , leo wameibuka na ushindi wa 2-1 dhidi KMC