MTANGAZAJI na mchambuzi maarufu wa masuala ya michezo nchini, Alex Kashasha ‘Mwalimu Kashasha’, amekiri kuwa kama Yanga itafanikiwa kumsajili kiungo nyota wa Klabu ya Simba, Clatous Chama,basi atawasaidia Yanga kutokana na ubora alionao.
Hivi karibuni kumekuwa na taarifa zinazomhusisha kiungo huyo wa Simba kuwa kwenye mazungumzo na uongozi wa Yanga ili kujiunga na timu hiyo.
Akizungumza katika mahojiano maluum ya +255 Global radio yaliyoruka mubashara kupitia Global TV Online, Kashasha alisema: “Kama ni kweli Yanga watafanikisha usajili wa Chama kama ambavyo tetesi zimekuwa zikieleza, basi utakuwa usajili bora, na naamini atakuwa msaada mkubwa kwao.”