Mzazi Aliyemuua Mtoto Wake Asakwa Na Polisi Jijini Mwanza





Tarehe 22.11.2020 Majira Ya 11:30hrs Huko Kata Ya Buswelu, Wilaya Ya Ilemela, Athuman Adam,  Miaka 10, Mkerewe, Mwanafunzi Wa Darasa La Tatu, Shule Ya Msingi Nyamadoke, Buswelu, Aliuawa Kwa Kile Kichodaiwa Kushambuliwa Na Fimbo Sehemu Za Mwili Wake Na Baba Yake Mzazi Aliyefahamika Kwa Jina La Adam Athuman, Miaka Kati Ya 30-40, Mkerewe, Fundi Ujenzi, Nyamadoke
Mtuhumiwa Huyo Baada Ya Kutekeleza Ukatili  Huo Alitoroka, Na Jeshi La Polisi  Linafanya Kila Jitihada Kuhakikisha Anatiwa  Nguvuni  Ili Afikishwe Kwenye Vyombo Vya Sheria. 

Mwili Wa Marehemu Umefanyiwa Uchunguzi Hospitali Ya Bugando Na Kukabidiwa Ndugu Kwa Mazishi.

Jeshi La Polisi Mkoa Wa Mwanza Linawaonya Na Kutoa Wito Kwa Wazazi Na Walezi Wote Kuwa Makini Na Aina Ya Adhabu Wanazotoa Kwa Watoto, Kwani Wanaweza Kujikuta Wakitenda Makosa Ya Kijinai Na Hatimaye Kufikishwa Mahakamani. 

Imetolewa Na;
Muliro Jumanne Muliro – ACP
Kamanda Wa Polisi (M) Mwanza
25, Novemba 2020


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad