Namna ya Kuachana na Matumizi ya Tumbaku na Sigara

 


Tumbaku ni moja ya mimea ambayo hapa kwetu Tanzania na katika mataifa mengine Duniani, mmea huu unazalishwa kama zao la biashara.


Matumizi ya zao hili kama zao la biashara inatokana na matumizi ya mmea huu katika kutengeneza sigara ambazo zimekuwa zikitumika kama kiburudisho kwa baadhi ya watu.


Uwezo wa tumbaku kutumika kama kiburudisho kwa baadhi ya watu, inatokana na mmea huu kuwa na kemikali ya asili ambayo hujulikana kwa jina la “Nicotine”.


Pamoja na kutumika kama kiburudisho kwa baadhi ya watu, tumbaku imekuwa na athari za kiafya ambazo zimepelekea kuwa na utaratibu wa matibabu ambayo yanajumuisha matumizi ya kemikali ambayo inapatikana katika tumbaku (Nicotine).


Baada ya kutumika mwilini (Tumbaku/Nicotine) hupelekea mabadiliko kadhaa kutokea katika mwili mfano, kuzalishwa kwa homoni (epinephrine) ambayo husababisha mishipa ya damu kusinyaa (constrictions of Arteries), moyo kushindwa kusukuma damu ili iweze kufika katika viungo vingine vya mwili pamoja na  mapigo ya moyo kuongezeka. Pia kemikali hii, nicotine husababisha vidonda (vidonda vya tumbo) na kupelekea vidonda kuchelewa kupona.


Pamoja na athari tajwa hapo juu za kiafya baada ya kutumia “nicotine”, pia matumizi yake yamepelekea utegemezi kwa mtumiaji “Nicotine Addiction”. Hali hii ya utegemezi imepelekea ugumu kwa baadhi ya watumiaji kushindwa kuacha uvutaji wa sigara au bidhaa zenye nicotine.


Kwa huduma au matumizi ambayo ni ya kitabibu, nicotine imekuwa ikitumika kama sehemu ya kumsaidia mtumiaji wa tumbaku au sigara kuweza kuacha matumizi hayo, “Recreational drug”.


Baadhi ya dawa ambazo zimeandaliwa kwa kutumia nicotine ni pamoja na zile zilizo katika maumbile ya daya ya kupuliza (nasal spray), kutafuna (nicotine gum), vidonge na pia dawa ya kuvuta (inhaler). Dawa hizi hutumika kumsaidia mtumiaji wa sigara au bidhaa zenye nicotine aweze kuacha uvutaji wa sigara au matumizi ya nicotine.


Kama ambavyo ilivyo kwa dawa nyingine ambazo zinatumika katika matibabu, huwa kuna muingiliano (interactions) wa dawa za aina tofauti pindi zinapotumika kwa pamoja katika mwili wa mtumiaji. Muingiliano huo yawezekana ukawa ni wenye manufaa kwa mtumiaji, au pia muingiliano huo yawezekana ukawa ni wenye kuleta madhara kwa mtumiaji.


Miongoni mwa dawa ambazo zinamuingiliano na nicotine/moshi wa tumbaku (bidhaa za tumbaku) katika matumizi ni pamoja na dawa zifuatazo:-


Dawa za kutibu matatizo ya moyo au shinikizo la damu (Propranolol), dawa za kisukari (Insulin), hii inatokana na nicotine kuwa na uwezo wa kuathiri namna ambavyo mwili unatawala kiwango cha sukari mwilini hususani katika uwezo wa insulin kufanya kazi. Dawa nyingine ambazo zinamuingiliano na nicotine ni dawa za pumu ambazo uwezo wa dama hizi unapungua endapo zitatumika sambamba na nicotine.


Pia, dawa za kutibu vidonda vya tumbo zitashindwa kufanya kazi kwa kiwango kinachohitajika kutokana na kemikali hii yenyewe kuwa na uwezo wa kumsababishia mtu apatwe na matatizo ya vidonda vya tumbo.


Pamoja na muingiliano huo wa nicotine na baadhi ya dawa, kemikali hii, nicotine imekuwa ikisababisha kupungua kwa hamu ya kula chakula kwa mtumiaji. Sababu hii imekuwa ikituiwa na baadhi ya watumiaji katika kutatua changamoto ya uzito mkubwa. Mtumiaji anatumia nicotine gum na bidhaa nyingine zenye kemikali hii katika kupunguza uzito wa mwili wake.


Kwa matumizi ambayo ni tahadhari kwa bidhaa jamii ya tumbaku/nicotine, haishauriwi nicotine kutumika kwa mama mjamzito. Tafiti zinaonyesha kwamba, wamama ambao wamekuwa ni watumiaji wa bidhaa zenye nicotine wamekuwa wakijifungua watoto ambao wanamatatizo katika baadhi ya viungo/maumbile ya miili yao.


Pamoja na tumbaku kuwa na kemikali aina ya nicotine ambayo imekuwa ikitumika katika mifumo mbalimbali ya matibabu, ni vyema kuzingatia faida na hasara za kemikali hii kabla ya kufanya matumizi yake.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad