Ndege mpya aina ya Bombardier itawasili nchini mwishoni December

 


Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Kampuni ya Ndege nchini (ATCL), Josephat Kagirwa, ameeleza kuwa ingawa hawajapata tarehe rasmi ya kuwasili kwake, lakini haitazidi mwisho wa mwezi ujao.


Kagirwa amesema hivi sasa wanasubiri taarifa ya mwisho ya kuwasili kwa ndege hiyo itakayokuwa na uwezo wa kubeba abiria 78.


Hadi sasa Serikali ya Awamu ya Tano imenunua ndege mpya 11, nane zimewashawasili, moja ni hiyo inayotarajiwa Desemba, mbili zinaendelea kutengenezwa nje ya nchi.


Kagirwa alisema ndege mbili zilizobaki aina ya Airbus A220-300 zenye uwezo wa kubeba abiria 132 zitawasili mwakani ikiwemo moja inayotarajiwa kuwasili katikati ya mwaka na nyingine mwishoni mwa mwakani.


Miongoni mwa ndege mpya ambazo Serikali ya Awamu ya Tano ilizinunua na tayari zipo hapa nchini zikiendelea na safari mbalimbali za ndani na nje ya nchi ni pamoja na Boeing 787-8 Dreamline mbili, Airbus A220-300 mbili na Bombardier Dash 8 Q400 nne.


Katika kuhakikisha ATCL inazidi kuimarika kwa kuwa na ndege za kutosha, Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 20.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad