NECTA Yatoa Ratiba ya Mitihani ya Kitaifa, 2020



Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza ratiba ya mitihani ya kidato cha pili ambayo itaanza kesho Novemba 9 hadi Novemba 20, 2020 katika shule za sekondari 4,948 Tanzania Bara.


Akizungumza na wanahabari leo Novemba 8, 2020 Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dkt. Charles Msonde amesema kuwa mwezi Novemba kila mwaka huwa ni mwezi wa upimaji na mitihani mbalimbali ya kitaifa, ambapo baada ya mitihani ya kidato cha pili itafuatiwa na mitihani ya kidato cha nne itakayoanza Novemba 23 hadi Disemba 11, 2020 kwa upande wa Tanzania bara na Zanzibar.


Wakati huo huo Dkt. Msonde amesema kuwa, mitihani ya darasa la Nne itafanyika Novemba 25 na 26, 2020 ambapo jumla ya shule za msingi 17,812 huku watahiniwa 1,825,679 wamesajiliwa kufanya upimaji huo wa kitaifa. Kati yao wavulana ni 909,068 sawa na asilimia 49.8 na wasichana ni 916,616 sawa na asilimia 50.2.


“Jumla ya 646,148 wamesajiliwa kufanya upimaji wa Kitaifa wa Kidato cha Pili, 2020 ambao kati yao wavulana ni 301,831 sawa na asilimia 46.71 na wasichana ni 344,317 sawa na asilimia 53.29. Aidha wapo watahiniwa wenye mahitaji maalum 731 na kati yao 406 ni wenye uoni hafifu, 55 ni wasioona, 3 wenye ulemavu wa kusikia na 267 ni wenye ulemavu wa viungo vya mwili”, amesema Dkt. Msonde

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad