Rapa #NickiMinaj ni miongoni mwa wahanga wa tuzo za #Grammy kufuatia kushindwa kutajwa kwenye kipengele chochote cha tuzo hizo 2021, licha ya kuachia album kali na ngoma iliyofanya vyema "Blinding Lights" mwaka huu.
Kupitia ukurasa wake wa twitter, #Nicki ameandika masikitiko yake akikumbusha pia alivyowahi kutendewa unyama na Grammy's.
-
"Sitasahau Grammys hawakunipa tuzo yangu ya Msanii Bora Chipukizi kipindi nilipokuwa na nyimbo 7 zinazofanya vizuri kwa pamoja kwenye chart za Billboard na pia rekodi ya kuwa msanii wa Kike wa Hip Hop aliyefanya vizuri kwenye wiki ya kwanza kuliko mwingine yeyote katika kipindi cha miaka 10. Pia kufanikiwa kushawishi kizazi. Walimpa msanii mweupe, Bon Iver." ilisomeka tweet ya #NickiMinaj.
#NickiMinaj ni miongoni mwa wasanii ambao hawajawahi kushinda #Grammy katika historia ya muziki wake licha ya kufanya mengi makubwa na mazito. Wengine ni Katy Perry, Busta Rhymes, Blake Shelton, Snoop Dogg, Nas, Tupac Shakur na wengine wengi.