Ntibazonkiza Afanya Balaa Huko Burundi, Apiga Bonge la Bao



KIUNGO mshambuliaji mpya wa Yanga, Mrundi, Said Ntibazonkiza, amethibitisha ubora wake kwa kuifungia timu yake bao la kusawazisha timu yake ya taifa ya Burundi ilipocheza dhidi ya Mauritania hivi karibuni.



Bao hilo alilifunga ugenini nchini Mauritania katika mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Mataifa Afrika (Afcon) ambalo lilitosha kuipa timu yake sare ya bao 1-1.

Mrundi huyo alifunga bao hilo kiufundi kwa njia ya faulo nje ya 18 baada ya kupiga mpira wa faulo ulioingia wavuni moja kwa moja bila kuguswa na mchezaji yeyote.

Ntibazonkiza ndiye aliyewahakikishia Burundi alama moja muhimu ugenini akifunga bao hilo ambapo baada ya mchezo huo, timu itarejea Burundi kuwakaribisha Mauritania.

Kiungo huyo ndio usajili mpya wa kwanza uliofanyika kwenye kikosi cha Yanga, atakayetua kuichezea timu hiyo baada ya kumaliza majukumu yake ya timu ya taifa.

Yanga imemsajili kiungo huyo kama mchezaji huru kutokana na kutokuwa na mkataba na klabu yoyote kufuatia kumaliza mkataba wake na Vital’O ya kwao Burundi.

Alisajiliwa na Yanga baada ya kuonyesha kiwango sambamba na kuifunga Taifa Stars ilipocheza mchezo wake wa kirafiki dhidi ya Burundi kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

Usajili wake ulipendekezwa na Kocha Mkuu mpya wa timu hiyo, Mrundi Cedric Kaze kutokana na kuufahamu uwezo wake wa kufunga na kutengeneza mabao.



Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad