Pacha wa Alikiba kutoka Zanzibar aibua mapya

 


Kuna ule msemo unasema duniani wawili wawili ikiwa ina maana mtu mmoja anaweza akawa na vinasaba vya kufanana na mtu mwingine kama alivyo ila tofauti huweza ikawa majina au jinsia tu.

 

Hii imetokea baada ya msanii anayefahamika kwa jina la Harith K maarufu kama pacha wa Alikiba au Kiba wa Zanzibar ambaye kimuonekano, matendo, kuongea, kuimba hadi kutembea anafanana na staa wa BongoFleva Alikiba.


Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital wakati anazungumzia suala hilo Harith K amesema alianza kumfuatilia Alikiba miaka 10 iliyopita na kwa bahati nzuri aliwahi kukutana na msanii huyo na alikiri kweli wamefanana.


"Alikiba alinipokea vizuri na ni mtu ambaye wa kawaida sana tofauti na wanavyomjaji na nimeanza kumfuatilia na miaka 10 iliyopita, kufanana na Alikiba ni kama zawadi kwa mungu nashukuru kwa hilo, mimi sitafuti kiki maana kama najifananisha naye ningeshaanza kuingia kwenye mitandao ya kijamii kujionyesha" amesema Harith K 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad