Pacha wa Mondi Aibua Mazito



BABA mzazi wa msanii mahiri wa Bongo fleva nchini, Nasib Abdul ‘Diamond Platinums’, Abdul Juma ‘Baba D’, ameibuka na kumkana kijana anayedai kuwa ndugu na mtoto wake huyo.

Kijana huyo aliyefahamika kwa jina la Chibu Rapper mwenye maskani yake Mwenge, Dar, ameibuka hivi karibuni na kujifananisha na staa huyo mkubwa wa muziki nchini.Habari na picha za pacha huyo zilianza kusambaa mitandaoni zikimfananisha Chibu Rapper na Mondi huku mashabiki wakipigia mstari kuwa wamefanana kweli.

CHIBU RAPPER AUNGANISHA DOTI


Chibu Rapper aliwahi kufunguka kuwa yeye amefanana na Mondi na kwenda mbali zaidi na kuongeza kuwa Mondi ni kaka yake kwa sababu ni mtu ambaye wamefanana kwa kila mtu.


“Mimi nafurahi sana kufananishwa na staa mkubwa kama Mondi, naweza kusema mimi ni pacha wake.


“Nimewahi kufuatwa hadi na wanawake wanasema mimi ni Diamond, nimeweza kupata fursa ya kuwa na wanawake wazuri kutokana na kufanana na staa huyu mkubwa.


“Nimewahi hata kupigwa na watu wakijua mimi ni Diamond, hata kwenye sherehe yake ya kuzaliwa huwa napata salamu nyingi tu za kupongezwa ndio maana huwa ninatamani sana kukutana na Diamond ili furaha yangu ikamilike,’’ alisema Chibu Rapper

BABA D AFUNGUKA

Baada ya kusambaa kwa picha na mahojiano ya kijana huyo akidai kuwa yeye ni pacha wa Mondi, baba mzazi wa Mondi, Baba D aliibuka na kusema kuwa hamjui kijana huyo na wala hana mtoto ambaye ni pacha wa Mondi japokuwa ni kweli amefanana na kijana wake.Akizungumza na AMANI, Baba D alisema kuwa Mondi hana pacha wake.

“Ni kweli ukimuangalia huyu kijana anafanana na Nasibu, japo si kwa kila kitu.

“Ila hakuna pacha wa Nasibu na kama ameamua kujitafutia ugali au riziki kwa njia hiyo ni sawa mi sina tatizo maana huo ni upendo pia kwa mwanangu.


“Kwa upande wa Nasibu mwenyewe akiamua kukutana naye na akamsaidia ni sawa tu haina shida,’’alisema Baba D.Hali hii imekuwa ikitokea kwa mastaa kufananishwa na watu wengine, kwani hata staa wa muziki wa Bongo Fleva na bosi wa Lebo ya Konde Gang Music, Rajab Abdul ‘Hramonize’, amewahi kufananishwa na mtu ambaye mpaka sasa anajiita Harmo Rapa.


Stori: Happyness Masunga na Khadija Bakari


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad