Nahodha wa klabu ya Liverpool, Jordan Henderson amepata maumivu kwenye mguu wake wa kulia na kushindwa kuendelea na mchezo wakati timu yake ya Taifa Uingereza ikicheza dhidi ya timu ya Taifa ya Ubeligiji na Uingereza Kufungwa mabao mawili kwa sifuri usiku wa hapo jana.
Maumivu aliyopata Jordan Henderson yanafanya orodha ya wachezaji wanaotumainiwa kwenye klabu ya Liverpool kufika tisa na kuzidi kumpasua kichwa kocha wa klabu hiyo Jurgen Klopp wakati akijiandaa kuwavaa Leicester City kwenye mchezo wa EPL Unaotaraji kuchezwa Jumapili ya wiki hii.
Kocha wa timu ya taifa ya Uingereza, Gareth Southgate amesema “Ni kweli Jordan amepata maumivu ya mguu na akahisi hawezi kuendelea na mchezo lakini hana uhakika kama ni kuchanika kwa nyama za paja”. Lakini atafanyiwa vipimo zaidi baada ya timu kurejea Uingereza, Aliongezea Southgate.
Wachezaji nyota tisa wa Liverpool wanaosumbuliwa na majeraha ni walinzi wote wa chaguo la kwanza, Virjil Van Dijk, Joe Gomez, Andy Robertson na Trent Alexander Anorld.
Viungo Fabinho, Thiago Alcantara, Alexander Oxlade Chamberlin na mshambuliaji Mohammed Salah ambaye ameripotiwa kupata maambukizi ya Ugonjwa wa Korona.