Polisi wa Uganda waizingira hoteli ya Bobi Wine

 


Police nchini Uganda wameizingira hoteli ambako mgombea wa urais nchini humo Robert Kyagulanyi, al maarufu Bobi Wine, katika mji wa Hoima magharibi mwa Uganda ambako ndiko alipo na maafisa maafisa wake wa kampeni.

Bobi ametuma ujumbe wake wa twitter akisema kuwa alilazimika kutumia njia ndefu kufika mjini humo baada ya wanajeshi kufunga barabara ambayo alitarajia kutumia.


"Wametufuata kwenye hoteli yetu na kuizingira ," alitweet.


Televisheni ya Uganda NTV alitweet ujumbe kuwa " lengo la operesheni hiyo bado halijajulikana ".


Bobi Wine alituma picha za polisi wakiwa nje ya hoteli alimokuwa:

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad