Polisi yaelezea suala la Lema kutishiwa maisha

Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Salum Hamduni, amesema kuwa aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la Arusha Mjini kupitia CHADEMA, Godbless Lema, hajawahi kutoa taarifa kama anatishiwa maisha na wala hakuna mtu yeyote aliyewahi kumtishia maisha yake.


Kauli hiyo ameitoa hii leo Novemba 9, 2020, wakati akizungumza kwenye kipindi cha SupaBreakfast ya East Africa Radio, hii ni baada ya taarifa kusambaa kwamba Lema anashikiliwa nchini Kenya, baada ya kuingia bila kuwa na nyaraka muhimu.


"Usalama wake hauko hatarini, yuko sawasawa tu na hakuna tishio lolote dhidi ya maisha yake", amesema Kamanda Hamduni.

Imeelezwa kuwa jana Novemba 9, 2020, Lema alishindwa kutoa nyaraka hizo muhimu kwa madai ya kuwa alikuwa anahofia maisha yake na kwamba alikuwa anaelekea nchini Kenya kwa ajili ya kutafuta hifadhi.

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huyu ni mbabaishaji Rastamani mgine.
    ni mmojawapo wa Genge la Uhamasishaji
    Maandamanoo yaliyo feli kwa Watanzania.

    Uso pa kuueka hana baada ya mbinu na mipango yao ovu kutaka kuliingiza taifa katika vurugu na uvunjfu wa amani ndio unaona kila mmoja anatafuta njia yake anajitoavipi..!!

    Mwingine chumbani kwa barozi na wengine wameripoti leo ostabe pia wako katika mchakato wa kusepa.

    Ruzuku kuikosa inauma. watasingizia mambo kemkem. Kukosa Ridhaa ya wananchi pia kumechangia, tena sana.

    Mazingira aliojitegenezea hayamfai.

    ReplyDelete
  2. Huyu kijana Godiless, alikuwa na Genge
    la Ki hashpapi mitandaoni,
    Hatuna uhakika kama BOT na benki zingine wamesalimika na kundi hili.

    Na pia sijuikama alikidhi matakwa ya kiafya na uhaiaji nchini kenya Kuhusu
    Covid-19 Certification. prior entry.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad