MCHEZAJI mkongwe wa Argertina, Diego Maradona, ametolewa hospitali siku ya Jumatano, na kuelekea kliniki ya kurekebisha tabia ili kuacha kutegemea pombe, Maradona, aliliongoza taifa lake katika mashindano ya Kombe la Dunia ya mwaka 1986.
Mapema mwezi huu alifanikiwa kufanya upasuaji katika ubongo ili kuondoa kuganda kwa damu.
Wakili wake amesema Diego amepitia kipindi kigumu zaidi katika maisha yake na ilikuwa kama miujiza kukuta damu imeganda katika ubongo wake na angeweza hata kupoteza maisha yake.
“Jambo zuri ni kuwa Diego yuko sawa sasa,” alisema wakili wake, Matias Morla, wiki iliyopita.
Maradona alilazwa katika kliniki ya Ipensa huko Buenos Aires, akiwa anasumbuliwa na anaemia (upungufu wa damu).
Baada ya upasuaji huo madaktari wamemshauri Maradona kuacha matumizi ya pombe ambayo yanaweza kuchukua uhai wake.