Pongezi kwa Ijumaa Kuondoa Kinyesi kwa Diamond Platnumz

 

MIEZI kadhaa iliyopita, mwanamuziki mkubwa barani Afrika, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ alitangaza hadharani kuzilipia kodi ya nyumba familia 500, jambo lililoleta kero kubwa mno kwa majirani zake, lakini sasa hali imekuwa shwari kwa kazi nzuri iliyofanywa na gazeti hili la IJUMAA.

Wakizungumza na Gazeti la IJUMAA, baadhi ya majirani wa Diamond au Mondi wanalishukuru na kulipongeza mno gazeti hili kwa kuandika habari iliyohusu kutapakaa kwa kinyesi cha binadamu kwenye mtaa wao wanaishi na Mondi, Mbezi-Beach jijini Dar.

Wiki nne zilizopita, Gazeti la IJUMAA lilifika kwenye mtaa huo na kukuta hali ni mbaya mno kufuatia umati wa watu waliokuwa wakifika maeneo hayo kutaka msaada kwa Mondi kujisaidia ovyo na kusababisha hofu ya mlipuko wa magonjwa kama kipindupindu.

“Wala tusiwe wanafiki, tangu mmeandika ile habari kwenye gazeti lenu (IJUMAA), sasa hivi hali imekuwa shwari kabisa hapa mtaani kwetu.


“Yal
e matukio ya watu kujisaidia ovyo, ubakaji na wizi yamepungua kwa kiasi kikubwa sana, wewe mwenyewe si umeona? Yaani siku hizi wale watu waliokuwa wanajazana hapo nje kwa Diamond wakijifanya kutaka msaada, tangu ile habari imetoka na wao hawapo kabisa.


 “Unajua ile habari ilivyotoka tu, viongozi wa mtaa wakaitisha kikao, ukawekwa ulinzi shirikishi, yaani sasa hivi mtu akionekana tu amezubaa hapa mtaani au nje ya nyumba ya Mondi, anafukuzwa ndiyo maana unaona hawapo.


“Kiukweli mmetusaidia sana Gazeti la IJUMAA.


“Hata kile kinyesi kilichokuwa kimetapakaa kwenye maeneo yetu, sasa hivi hakipo, yaani ukikuta ni mara chache sana kwa sababu walivyofukuzwa kuna wengine tumesikia walikimbilia baharini huko,” anasema mmoja wa majirani wa Mondi aliyeomba hifadhi ya jina gazetini.

 

Katika habari hiyo ya ukurasa wa mbele iliyosomeka; MAKAZI YA MONDI YATAPAKAA KINYESI, baadhi ya majirani na viongozi wa serikali ya mtaa walionesha kukerwa na hali hiyo. 


Mbali na kinyesi kuzidi kuwa kero kwa wakazi wa eneo hilo, pia vitendo vya wizi na ubakaji vilitawala maeneo hayo, jambo lililozidi kuwapa hofu majirani hao, lakini kwa sasa hali ni shwari.


Stori: Memorise Richard

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad