Putin na Rais wa Mexico Wagoma Kumpongeza Joe Biden

 


Wakati marais na viongozi mbalimbali wameendelea kumpongeza Joe Biden kwa ushindi wa Urais Marekani, Marais wa Urusi Vladimir Putin na wa Mexico Andres Lopez wamesema bado ni mapema mno kumpongeza Joe kwa kuwa bado Mgombea Urais kupitia Chama cha Republican Donald Trump, hajakubaliana na matokeo hayo.


Rais Putin amesema atatoa pongezi kwa mshindi wa Urais wa Marekani “Tumeona ni busara kusubiri pande zote zikubaliane na matokeo, yeyote atakayetangazwa mshindi, tutaheshimu maamuzi ya wamarekani walio wengi” .


Kwa upande wake rais wa Mexico Andres Lopez amesema ”Lazima tuheshimu haki za watu, bado kuna upande wa Trump una lalamiki matokeo, binafsi sitoi pomgezi, nitasubiri hadi mambo yote ya kisheria yashughulikiwe”.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad