Rage Ampa Mbinu Sven Kuwavaa Plateau




ALIYEWAHI kuwa mwenyekiti wa klabu ya Simba, Ismail Aden Rage amempa tahadhari kocha wa timu hiyo, Sven Vandenbroeck kuhakikisha anakwenda katika mchezo wao wa Jumamosi dhidi ya Plateau United ya Nigeria kwa tahadhari.

 

Simba itashuka dimbani siku ya Jumamosi kuvaana na Plateau United katika mchezo wa awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika huku mchezo wa marudiano ukitarajiwa kupigwa kati ya Desemba 4-6.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Rage amesema, timu ya Simba ina rekodi nzuri katika michuano hiyo lakini ina historia mbaya na timu za Nigeria ambazo mara nyingi wakikutana nazo wanawaondoa.



“Sina matatizo na Simba katika michuano hii ya ligi ya mabingwa kwani tuna rekodi nzuri huko nyuma, sisi ndio timu ya kwanza kutwaa Kombe la Cecafa mwaka 1974, pia mwaka huohuo tulifanikiwa kuweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kufika nusu fainali ya klabu Bingwa Afrika katika ukanda wetu, hivyo sina shida nayo.

 

“Lakini kocha anatakiwa kwenda kwa tahadhari kubwa kuelekea mchezo huo kwani tuna historia mbaya na timu za Nigeria kila tukipangiwa kwani tumekuwa hatuvuki mbele yao, hivyo wanahitaji kuwa na maandalizi ya kutosha kuelekea mchezo huo.

“Lakini kwa safari hii jinsi kikosi kilivyo nina imani tutafanikiwa kuvuka, kikosi kipo vizuri,” alisema Rage.

Khadija Mngwai, Dar es Salaam


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad