Raia mmoja wa Indonesia amebahatika kuwa milionea baada ya jiwe la thamani kuangukia nyumba yake kutoka angani.
Josua Hutagalung ambaye ni mkazi wa eneo la Sumatra Kaskazini, aliliuza jiwe hilo la thamani lenye uzito wa kilo 2.1 kwa mtaalamu wa mikusanyiko ya makavazi wa Kimarekani Jay Piatek.
Jiwe hilo la thamani lililouzwa kwa fedha pauni milioni 1.4, linakadiriwa kuishi kwa miaka bilioni 4.5.
Jiwe hilo limebainishwa kuwa jamii ya nadra kwa muundo wake uliotokana na madini adimu aina ya CM1/2 Carbonaceous Chondrite.