Rais Magufuli Akiri Ugumu wa Kuteau Mawaziri



Rais Dk. John Magufuli amesema kazi ni ngumu kwenye kuteua baraza la mawaziri kutokana na kila mmoja kuwa na vigezo.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Novemba 16, kwenye hafla ya kuwaapisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango iliyofanyika ikulu jijini Dodoma.


"Kwanza ni lazima nikiri kwamba sikuwa na haraka sana ya kuteua baraza la mawaziri na nyie wabunge ni mashahidi kwamba mwaka huu tunawabunge zaidi ya 350 na bado wabunge was nafasi zile 10, sasa sikutaka niteue harakaharaka.


"Na mimi ningeomba wabunge presha mzishushe sababu kazi tuliyoomba hapa ni ubunge wala siyo uwaziri, tulitoka hapa wengine mlikuwa wabunge kwenda kuomba ubunge kwamba tutawatumikia wananchi wetu na tukakabidhiwa ilani ya uchaguzi yenye kurasa 303 sasa mengine yanatoka wapi?


"Hivyo ni suala ambalo halihitaji haraka, kwa hiyo nawaomba sana wabunge najua maneno ni mengi, kwa kwa waganga nendeni shauli yenu, wengine watawapaka mikosi lakini najua hamuendi," amesema Rais Magufu.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad