Rais Magufuli Awatoa Hofu Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya......."Chapeni Kazi, Msiwe na Wasiwasi"



Rais Dkt. John Magufuli amewataka wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kuondoa hofu za kutenguliwa kutoka kwenye nafasi zao.

Dkt. Magufuli ameyasema hayo leo wakati akitoa hotuba yake mara baada ya kumuapisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Adelardus Kilangi, Ikulu Chamwino jijini Dodoma.


Rais Dkt. Magufuli amesema kuwa yanapotajwa mafanikio ya Serikali iliyopita viongozi hao hawawezi kukosekana hivyo waondoe shaka kwani hafikirii kuteua viongozi wapya kwenye nafasi hizo.


“Nashangaa napata vimeseji vingine, ‘Mheshimiwa Rais nimejitahidi katika kipindi changu’ kana kwamba kipindi chake nilimwambia kinaisha baada ya mimi kuapishwa.


“Nimeona hili nilizungumze, kwamba wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya msiwe na wasiwasi, na inawezekana wala pasitokee mabadiliko hata moja, labda kwa mtu atakayestaafu au atakayefanya mambo ya hovyo sana.”


Aidha, Rais ametoa wito kwa watendaji wa Serikali kuchapa kazi.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad