Rais Magufuli Kuzindua Bunge Novemba 13


Rais wa Tanzania,  John Magufuli atalihutubia Bunge la 12 Ijumaa Novemba 13, 2020 huku wabunge ambao wapo nje ya Dodoma wakitakiwa kurejea jijini humo.

Spika wa Bunge, Job Ndugai ameeleza hayo bungeni leo Jumatano Novemba 11, 2020 wakati akitoa taarifa kwa wabunge kabla kuanza kwa shughuli za kikao cha pili.

Ndugai amesema kila mkutano wa kwanza wa Bunge jipya rais anahutubia ili kuweka dira ya Serikali kwa miaka mitano inayokuja na utekelezaji wa ilani kadiri anavyoona inafaa.

Amesema kwa kuwa hutuba hiyo ni muhimu amewataka wabunge ambao wana mpango wa kusafiri nje ya Dodoma kuahirisha safari zao.

“Hata wale ambao wapo nje ya Dodoma wanatakiwa kurejea ili kusikiliza hutuba hiyo. Sisi wabunge saa tatu kamili tuwe ndani ya ukumbi huu, tunaomba sana kuwahi kufika nikisema saa tatu kamili uwe kwenye kitu ni kwamba uwasili saa mbili. Siku hiyo tutakuwa na wageni wengi, kutakuwa na gwaride hapo nje,” amesema Ndugai.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad