Rais wa zamani Mali Amadou Toumani Toure aaga dunia



Rais wa zamani wa Mali Amadou Toumani Toure, ambaye aliliongoza taifa hilo katika eneo la Sahel kwa miaka 10 kabla ya kuondolewa mamlakani, amefariki leo nchini Uturuki.              


  Kiongozi huyo wa zamani wa Mali alikuwa na umri wa miaka 72. Daktari wake na mwanafamilia ambaye ni mpwa wake Oumar Toure wameeleza kwamba Amadou Toumani Toure alifariki usiku wa kuamkia leo nchini Uturuki, ambako alikuwa amepelekwa kwa ajili ya matibabu. Rais huyo wa zamani wa Mali Jenerali AmadouToumani Toure, atakumbukwa kwa jitihada zake za kuleta mageuzi ya kidemokrasia nchini mwake kabla ya kuangushwa kwenye mapinduzi ya kijeshi mnamo mwaka 2012.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad