Rais wa zamani wa Honduras azuiwa uwanja wa ndege akiwa na begi la pesa



Rais wa zamani wa Honduras Manuel Zelaya amesema alizuiwa katika uwanja wa ndege wa mji mkuu wa Tegucigalpa akiwa na dola 18,000 kwenye begi lake. Zelaya amesema aliachliwa huru masaa matatu baade, kulingana na gazeti la nchini humo La Tribuna. 
Katika ukurasa wake wa Twitter alidai kuwa pesa hizo sio zake, na alikuwa amepanga kwenda nchini Mexico kwenye semina. 

Kulingana na sheria za Honduras, msafiri yoyote anaruhusiwa kubeba sio zaidi ya dola za Kimarekani 10,000. 

Akiwa amezuiwa katika uwanja huo wa ndege, nje kulizuka maandamano ya raia. Kulingana na vyombo vya habari polisi walilazimika kutumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya. 

Zelaya alihusika katika biashara ya mbao kabla ya kuwa rais wa Honduras mwaka 2006.

 Alitimuliwa madarakani mwaka 2009. Na sasa ni kiongozi wa chama cha siasa za mrengo wa kushoto cha Libre.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad