Rais wa zamani wa Korea Kusini ahukumiwa miezi nane jela

 


Mahakama ya Korea Kusini imemkuta na hatia na kumhukumu kifungo cha miezi minane, rais wa zamani wa nchi hiyo Chun Doo-Hwan ya kumchafulia jina mwanaharakati wa zamani wa kutetea demokrasia aliyehusika kuipinga serikali ya rais huyo katika miaka ya 1980. 

Kesi hiyo ilisimamishwa kwa miaka miwili na kwa maana hiyo rais huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 89 huenda asitumikie kifungo hicho jela. 


Kesi hiyo imefanyika katika mahakama ya mji ulioko Kusini Magharibi wa Gwangju, ambako mamia ya watu na pengine maelfu inaaminika waliuwawa wakati raia walipoamua kusimama kidete dhidi ya serikali ya kimabavu ya Chun mnamo mwaka 1980 na kukabiliwa na nguvu kubwa ya polisi na vikosi maalum pamoja na vifaru.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad