Rayvanny Apewa Ufalme wa Harmonize

 


KUMEIBUKA mjadala mkali juu ya ni msanii gani wa Bongo Fleva mwenye mafanikio zaidi kati ya Rajabu Abdul ‘Harmonize’ na mwenzake, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’?


Katika mjadala huo mkali kati ya mashabiki wao, Rayvanny amejikuta akipewa ufalme anaopewa Harmonize au Harmo.

 

Ikumbukwe kwamba, jamaa hawa walikuwa washindani wakubwa tangu walipokuwa kwenye lebo moja ya Wasafi Classic Baby (WCB) chini ya Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kabla ya Harmo kujitoa mwaka jana na kwenda kuanzisha lebo yake ya Konde Gang Music Worldwide.

 

“Ukubwa wa msanii unatokana na idadi ya tuzo za ndani na nje (za kimataifa).


“Sasa ukubwa wa Harmonize upo wapi mbele ya Rayvanny?


“Harmonize tunajua ana tuzo moja tu tangu atambulike kwenye muziki. “Kumiliki lebo hakumfanyi Harmonize aonekane mkubwa, ukubwa wa msanii unachangiwa na tuzo.

 

“Mimi naweza kusema Rayvanny ni bora kuliko Harmonize kwa sababu ameshinda tuzo ambazo mpaka sasa ni zaidi ya saba na zote ni za kimataifa.


“Ukienda kwenye mitandao ya kijamii, ukiondoa Instagram, kwingine kote Rayvanny amempiga bao Harmonize kwa kuwa na fanny-base kubwa (mashabiki wengi).

 

“Angali upande wa YouTube ambapo Harmonize anadai hakuchangii msanii kuonekana ni bora zaidi, lakini Rayvanny amemzidi kwa subscribers (wafuasi) karibia milioni moja.


“Suala la kujitegemea nje ya lebo halichangii msanii kuwa mkubwa.

 

“Nikujuze tu kwamba tuzo pekee ya Harmonize aliichukua kupitia wimbo alioshirikiana na Diamond wa Bado ila upande wa Rayvanny tukiitoa Tetema iliyompatia Tuzo ya Video Bora Afrika, ana tuzo nyingine kama sita ambazo amechukua kupitia ngoma zake mwenyewe ikiwemo ile kubwa ya BET.

 

“Angali sasa hivi, Rayvanny yupo kwenye nominations (wanaowania) kwenye tuzo kubwa duniani za Grammy, wakati Harmonize hajatajwa,” anasema rafiki wa karibu wa wasanii hao huku akiungwa mkono na wenzake ambao ni wasanii chipukizi waliokuwa wakipiga stori na Gazeti la Ijumaa.

 

Akizungumzia mafanikio ya Rayvanny, Mondi anasema kuwa, kwa sasa msanii huyo amekua na hivi karibuni yupo mbioni kuanzisha lebo yake kwani tayari ana studio kubwa na ya kisasa kuliko studio zote Bongo.

 

“Studio ya Rayvanny ni kubwa zaidi ya studio zote hapa Tanzania. Hakuna anayezuiwa kuanzisha lebo ndani ya Wasafi, hata Drake ana lebo yake, lakini yupo kwenye Lebo ya Cash Money,” anasema Mondi akizungumzia mafanikio ya Rayvanny.


STORI: HAPPYNESS MASUNGA

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad