Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila, ameamuru watu sita kukamatwa na kufikishwa Mahakamani baada ya kubainika kughushi sahihi za watu wawili waliofariki dunia na kuiaminisha Serikali kuwalipa fidia ya Shs. Mil. 108 katika eneo lenye mradi wa soko.
Chalamila amefikia hatua hiyo baada ya kufanya mkutano wa hadhara katika mtaa wa Ikuti kata ya Iyunga Jijini humo, ambapo kuliibuka mgogoro wa eneo la soko ambalo watuhumiwa walikuwa wakidai ni mali yao walikuwa wakimiliki na kujenga kilabu cha pombe cha wazee wakati huo jiji likiwa limewalipa milioni 17.