Samatta Aumia, Nje ya Uwanja Siku Kumi



Na Zainab Nyamka, Michuzi Tv


MSHAMBULIAJI wa Timu ya Taifa ya Tanzania na Fenerbache, Nahodha Mbwana Ally Samatta atakuwa nje ya dimba kwa muda wa siku 10 baada ya kuumia.


Samatta amepata maumivu ya misuli katika mchezo wake wa mwisho wa Ligi ya Uturuki   dhidi ya Konyaspor wakipoteza kwa goli 2-0.


Baada ya maumivu hayo, Samatta ataukosa mchezo wa kufuzu AFCON kati ya timu yake ya Taifa Tanzania dhidi ya Tunisia utakaochezwa Novemba 13 na Novemba 17 mwaka huu.


Kwa upande wake Samatta amesema,  aliumia katika mechi ya mwisho ya Ligi na alipata maumivu ya misuli na nilifanyiwa vipimo na majibu yametoka mabaya kwahiyo atakuwa nje kwa siku zaidi ya 10.


Amesema, ripoti ya daktari inaelezea kuwa anatakiwa apumzike ili misuli irejee  katika hali ya kawaida.


 Samatta ametoa ya moyoni na kusema, ameumizwa sana kuukosa mchezo huo muhimu kwani alitamani awepo uwanjani kama kiongozi wa timu ila haina jinsi na ameenda kuongea na vijana wa timu pamoja na viongozi ili kuwapa morali ya ushindi.


Kwa sasa timu ipo nchini Uturuki ikijindaa na mchezo wao wa kufuzu AFCON dhidi ya Tunisia.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad