Mshindi mara nne wa tuzo ya mchezaji bora Afrika Samuel Eto’o amenusurika katika ajali siku ya Jumapili wakati akielekea mji wa kibiashara nchini Cameroon wa Douala, kwa mujibu wa wanafamilia wake.
Alikuwa akirejea kutoka mji wa Bafoussam, Magharibi mwa Cameroon, ambako alihudhuria tamasha mwishoni mwa juma.
Dereva alisema kuwa alishindwa kulidhibiti gari na kuyagonga magari mawili yaliyokuwa kwenye msafara wa Eto’o.
Msemaji wake alizungumza na BBC idhaa ya Pidgin kuwa anaendelea vizuri na kuwa gari lake liliharibika.
Alikataa kujibu maswali zaidi.