Serengeti Yapewa Tuzo ya Hifadhi Bora Barani Afrika



Moja ya taarifa ya kuifahamu leo November 10, 2020 Hifadhi za taifa ya Serengeti imeshinda tuzo ya kuwa hifadhi bora katika bara ya Afrika kwa mwaka 2020.


Katika taarifa iliyotolewa na Kamishna msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi- Mawasiliano, Pascal Sheltete, imesema tuzo hizo zimetangazwa jana Novemba 9, 2020 na taasisi ya World Travel Awards (WTA) ya nchini Marekani kwa njia ya Mtandao.




Taarifa hiyo imesema kuwa hii ni mara ya pili kwa hifadhi ya taifa ya Serengeti kushinda katika kundi la hifadhi zinazoongoza kwa ubora zaidi bara la Afrika.


“Serengeti imeibuka na ushindi katika shindano hilo lililoshindanisha hifadhi nyingine za central kalahari  ya Botswana,  Etosha ya Namibia, Kidepo Valley ya  Uganda Kruge ya Afrika Kusini na Masai Mara National Reserve ya Kenya.”


Imeeleza kuwa Serengeti inajivunia umaarufu wa Msafara wa Nyumbu uhamao zaidi ya milioni Moja na nusu,aina mbalimbali za wanyama pori wanaopatikana kwa wingi, maadhari nzuri ya kuvutia pamoja na shughuli mbalimbali za utalii zinazovutia watalii wengi.


Aidha TANAPA imeishukuru serikali, wananchi, wadau wa utalii pamoja na watu wote waliotumia muda wao kupiga kura na kuifanya serengeti kuwa mshindi wa hifadhi boara zaidi kwa bara la Afrika 2020. 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad