Shinyanga: Muuguzi aliyeiba vifaa vya Mil. 26 akamatwa




Muuguzi wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Shinyanga, Madaraka Joseph(32), pamoja na Dkt. Suka Charles(42), ambaye ni mmiliki wa Dispensary iliyopo wilayani Kahama, wanashikiliwa na Jeshi la polisi kwa tuhuma za wizi wa mashine mbili za kuangalia wagonjwa katika chumba cha upasuaji.



Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, Debora Magiligimba.


Taarifa hiyo imetolewa leo Novemba 7, 2020, na Kamanda wa Polisi mkoani humo, Debora Magiligimba, na kusema kuwa wizi wa mashine hizo pamoja na vifaa vyake vya hospitali ya mkoa wa Shinyanga, ulifanyika Oktoba 13 mwaka huu na baada ya kufanya uchunguzi walifanikiwa kupata vitu hivyo vikiwa nyumbani kwa Dkt.Suka maeneo ya Mhongolo Kahama.


Kamanda Magiligimba ameongeza kuwa, Dkt. Suka, alipohojiwa alidai kuuziwa vifaa hivyo na muuguzi wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Shinyanga, Madaraka Joseph, ambaye ni mfanyakazi wa chumba cha upasuaji kwa makubaliano ya kulipwa shilingi milion 4 na tayari alikuwa ametanguliziwa shilingi milioni 2.


Kwa mujibu wa Eatv.tv Kamanda Magiligimba amesema mashine mbili za kuangalia wagonjwa chumba cha upasuaji, zilizoibiwa ni pamoja na Edani 1M8 na Data Scop 1 zikiwa na vifaa vyake vyote vyenye thamani ya shilingi milioni 26, ambapo watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika ili kujibu tuhuma zinazowakabili.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad