Simba Ngoma Ngumu...Yashindwa Kumtwanga African Sports, Watoshana Nguvu

 

KIKOSI cha Simba leo kimalazimisha sare ya bila kufungana na timu ya African Sports kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Chini ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck leo langoni alikaa kipa namba tatu, Ally Salim na kuliweka lango lake salama ndani ya dakika 90.

Kwa upande wa safu ya ushambuliaji chini ya nyota Charlse Ilanfya imeshindwa kufurukuta kupata bao mbele ya Klabu ya African Sports.

Sven amefanya mabadiliko makubwa kwenye kikosi cha leo ambapo amewatumia vijana wengi chini ya miaka  20 ili kuwapa uzoefu.

Miongoni mwa nyota hao ni pamoja na Hassan Mohamed,Omary Kazi, Isack Mohamed, Godfrey Mbomahenga, Seif Suleman na Hamis Manguka.

Wale wa kikosi cha kwanza ilikuwa ni pamoja na kiungo Clatous Chama,Francis Kahata, Ibrahim Ame, Kened Juma, Miraj Athuman, Rarry Bwalya na Beno Kakolanya. 

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad