Sirro aagiza operesheni kufanyika maeneo haya



Mkuu Wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro, amewaagiza makamanda wote nchini kuhakikisha wanafanya operesheni  kwenye maeneo yote wanaokusanya vyuma chakavu, ili kubaini watu wanao hujumu miundombinu ya reli ya mwendokasi na wawezwe kuchukuliwa hatua



IGP Sirro ameyasema hayo wakati alipofika Kituo cha pollisi Mlandizi, akitokea Dar es Salaam, alipokutana na viongozi wa reli baada ya kupatiwa taarifa ya wizi wa vyuma hivyo ambavyo inaweza kuleta madhara makubwa endapo Kama huduma ya reli zimekwisha anza.


Aidha IGP Sirro amewaonya watanzania kuachana na tabia ya kujihusisha na tabia za kuchukua vyuma vya reli kwani watakuwa wamejiingiza kwenye matatizo makubwa.


Sambamba na haya IGP sirro ameuomba uongozi wa reli kuwapatia elimu askari wa Jeshi la Polisi ili iwe rahisi kwao   kufahamu nyaraka  na  kuweza  kufanya ukaguzi kwa umakini zaidi.


Tukio lililotokea eneo la ruvu darajani, Wilaya ya kipolisi Mlandizi ambapo askari walilikamata gari aina ya  Fuso yenye namba za usajili T167 DJW likiwa limebeba vyuma chakavu vikiwa vimechanganywa na vyuma vya reli ya Mwendokasi ndilo lililobainisha wizi huo wa vyuma vya Reli.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad