Tanasha Amfuata Zari Nyumbani kwa Mondi...Kisa Mtoto Wake Naye Ale Bata na Wenzake

 


KAMA noma na iwe noma! Ndivyo unavyoweza kuzungumza kufuatia taarifa mpya kutoka Kenya kudai kuwa, mwanadada Tanasha Donna Oketch naye anatarajia kuibuka Bongo, nyumbani kwa mzazi mwenzake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ au ‘Mondi’, IJUMAA WIKIENDA limenasa mchongo mzima.


ANAFUATA NINI?

Kama ilivyokuwa kwa Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, taarifa inaeleza kuwa, naye atamleta mwanawe Naseeb Junior kwa baba yake, ale bata kama wenzake, Tiffah Dangote na Prince Nillan.


Taarifa hiyo imekuja ikiwa ni siku chache tu tangu mwanamama Zari atie maguu Bongo akiwa ameambatana na watoto wawili aliozaa na Mondi, Tiffah na Nillan.

GUMZO KAMA LOTE

Baada ya Zari kutia timu, gumzo kama lote liliibuka kwenye mitandao ya kijamii kufuatia bibie huyo kumfungia vioo Mondi kwa takriban miaka miwili tangu waachane siku ile ya Wapendanao (Vallentine’s Day) ya Februari 14, 2018.

MASWALI YA WENGI

Maswali ambayo yalihojiwa na wengi kwenye mitandao ya kijamii ni haya; Zari amefuata nini kwa Mondi? Wamerudiana? Wamelala chumba kimoja? MAJIBU YA ZARI Kwenye mahojiano aliyoyafanya mara baada ya kufi ka, Zari alisema hajarudiana na Mondi, bali kilichomleta Bongo ni suala zima la kulea watoto (co-parenting).

TURUDI KWA TANASHA SASA

Kitendo cha Zari ‘kutrendisha’ mitandao ya kijamii ndicho kilichotajwa kuwasukuma waandishi wa nchini Kenya kumuuliza Tanasha amelipokeaje suala hilo na ndipo inaelezwa kuwa, alisema haoni kama ni tatizo na hata yeye atamleta mwanaye kwa Mondi.

KIROHO SAFI

Imeelezwa kuwa, mtu wa karibu na Tanasha aliyefi kiwa na waandishi hao wa mitandao ya Kenya amesema kuwa, Tanasha haoni tatizo Zari kutua nyumbani kwa Mondi na watoto kwani watoto ni haki kulelewa na wazazi wote wawili bila kujali kama wazazi walishaachana.


“Amesema hata yeye (Tanasha) ataenda Bongo nyumbani kwa Mondi) siku si nyingi kumpeleka mwanaye kwani jambo ambalo linatakiwa katika kuhakikisha mnawapa watoto haki yao ya malezi,” alinukuliwa mtu huyo aliye karibu na Tanasha.

ANARUDISHA MAJESHI?

Mtu huyo alisema kuwa, Tanasha ana maisha yake kwa sasa hivyo kitakachomleta kwa Mondi ni mtoto huyo waliyezaa pamoja kisha kuachana na si vinginevyo.

“Wala hana hata mpango na Mondi tena kwa sasa, ana maisha yake mengine tofauti. Kama Zari atakuwa ametumia kigezo cha watoto kwa lengo la kurudiana na Diamond atakuwa ni yeye, lakini si kwa Tanasha,” alimaliza shosti huyo wa Tanasha.

UONGOZI WA MONDI

Ukizungumza na Gazeti la IJUMAA WIKIENDA, uongozi wa Diamond kupitia kwa meneja wake, Said Fella ‘Mkubwa Fella’ umesema kuwa, hawawezi kusema kama ilikuwa kazi rahisi au ngumu kumrudisha Zari kwa msanii wao.

HUYU HAPA MKUBWA FELLA

“Unajua siwezi kusema kwamba tulitumia nguvu nyingi sana kumfanya Zari aje Bongo, wala siwezi kusema kuwa hatukutumia nguvu yoyote ile.

“Kwa sababu tunaweza tukatumia nguvu kubwa kuwapatanisha, lakini wao wakawa hawako tayari, vilevile tunaweza tusitumie nguvu yoyote kuwaweka pamoja, lakini mwisho wa siku ukawakuta wapo wote.

“Tulijaribu kwa uwezo wetu kuzungumza nao na kwa kuwa wao ni watu wazima na wanajua nini wanafanya, basi walituelewa, walikaa chini, wakazungumza na kuona kile walichokuwa wanakifanya hakikuwa sahihi.

“Ndiyo maana leo hii unaona Zari amewaleta watoto nchini kwa ajili ya kumuona baba yao na furaha imerejea upya,” alisema Mkubwa Fella na kuongeza;

“Sisi kama viongozi tumefurahi sana kuona familia imerudi kama zamani kwa sababu furaha ya Diamond ndiyo furaha yetu sisi, miaka miwili bila kuwaoana watoto wake si mchezo, hivyo kwa sasa tegemeeni kuona mambo makubwa katika muziki wake pia.”

WAMERUDIANA RASMI?

Alipoulizwa kama anamaanisha wawili hao wamesharudiana au wanalea tu watoto pamoja kama wazazi? Mkubwa Fella alijibu; “Hilo mimi sijasema, hayo mengine tuwaachie wenyewe ndiyo wanajua ukweli.”

TUJIKUMBUSHE

Miaka mitano iliyopita, Mondi alianzisha uhusiano wa kimapenzi na mwanamama Zari, raia wa nchini Uganda baada ya kutoka kuachana na aliyekuwa mpenzi wake, Wema Isaac Sepetu.

Zari na Mondi walibahatika kupata watoto wawili ambao ni Tifah na Nillan na baada ya muda penzi lao likaingia doa na kusababisha mwanamama huyo kwenda kuweka kambi maskani kwake, Afrika Kusini na wanawe.

AZAA NA TANASHA

Wakati wametangaza kuachana, baadaye Mondi alikinasa kifaa kipya (Tanasha) kutoka nchini Kenya na wakaanzisha safari mpya ya malovee ambapo walifanikiwa kuzaa mtoto mmoja kisha wakamwagana.

MAGAZETI PENDWA YALIANDIKA…

Habari ya watoto wa Mondi kuja Bongo ilikuwa ya kwanza kuandikwa na Magazeti Pendwa ya Global Publishers ambapo magazeti hayo yalipata taarifa hiyo miezi kadhaa iliyopita. Taarifa hizo ambazo zilichapishwa kwenye magazeti hayo, zilieleza wazi kuwa, Zari ana mpango wa kuwaleta watoto hao waje kumuona baba yao, lakini walishindwa kutokana na masharti makali ya ugonjwa wa Corona yaliyokuwa yamewekwa hasa nchini Afrika Kusini.

STORI: MEMORISE RICHARD, DAR

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad