Ulaji wa udongo kitaalamu hufahamika kama Geophagy. Kula udongo huhusishwa na upungufu wa Madini Chuma Mwilini na mara nyingi huonekana kwa Wajawazito
Ulaji wa Udongo umefanyika kwa miaka mingi sana mpaka sasa ingawa hutofautiana kwa Nchi na Nchi, na imeonekana kuwa tabia ya kawaida hasa kwa Wajawazito
Ni mara chache sana Daktari kumshauri Mgonjwa au Mjamzito kula udongo, kwasababu ingawa Udongo unaweza kusaidia lakini pia, unaweza kubeba sumu na kuhatarisha Maisha ya mhusika.