The Weeknd ni muhanga wa tuzo za Grammy, ameibuka na kuwatupia lawama kwamba ni wala rushwa mara baada ya jina lake kukosekana kwenye vipengele vyote vya tuzo hizo.
Licha ya kuachia moja ya album kubwa za mwaka huu 'After Hours' jina la mwimbaji huyo raia wa Toronto Canada halijatajwa miongoni mwa wasanii watakaowania tuzo za Grammy 2021. Kupitia ukurasa wake wa twitter, The Weeknd amewashutumu kwa kashfa za rushwa na kuomba uwazi katika uteuzi
-
"Grammy wanabaki kuwa wala rushwa, ninawadai, mashabiki zangu na kiwanda kizima tunahitaji uwazi." ilisomeka tweet ya The Weeknd.
Harvey Mason ni miongoni mwa wana jopo la Recording Academy ambalo uhusika kwenye kuchuja na uteuzi wa majina ya wasanii kuingia kwenye vipengele, amezungumza na mtandao wa Variety na kulizungumzia hili la The Weeknd.
Amesema The Weeknd aliwasilisha album yake kwa mapendekezo hivyo bodi ndio yenye maamuzi ya kupitisha kilicho sahihi, majina ni nane tu yanayohitajika kwenye kipengele cha vikubwa kama Album bora, Wimbo bora, Msanii Chipukizi.